Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 11 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ هَمَّ قَوۡمٌ أَن يَبۡسُطُوٓاْ إِلَيۡكُمۡ أَيۡدِيَهُمۡ فَكَفَّ أَيۡدِيَهُمۡ عَنكُمۡۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ﴾
[المَائدة: 11]
﴿ياأيها الذين آمنوا اذكروا نعمة الله عليكم إذ هم قوم أن يبسطوا﴾ [المَائدة: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, yakumbukeni yale Aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu, miongoni mwa neema ya usalama, kutia uoga kwenye nyoyo za maadui zenu waliotaka kuwavamia, Mwenyezi Mungu Akawaepusha na nyinyi na Akaweka kizuizi kati yao na yale waliyoyataka kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, muwe na hadhari naye. Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, katika mambo yenu ya kidini na ya kidunia na muwe na hakika ya kupata msaada Wake na uokozi Wake |