Quran with Swahili translation - Surah Qaf ayat 30 - قٓ - Page - Juz 26
﴿يَوۡمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ ٱمۡتَلَأۡتِ وَتَقُولُ هَلۡ مِن مَّزِيدٖ ﴾
[قٓ: 30]
﴿يوم نقول لجهنم هل امتلأت وتقول هل من مزيد﴾ [قٓ: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Watajie watu wako, ewe Mtume, Siku tutakayoiambia Jahanamu, «Je umeshajaa?» Na Jahanamu iseme, «Je kuna nyongeza yoyote ya majini na binadamu?» Hapo Mola, uliotukuka utukufu wake, Aweke unyayo Wake ndani yake, na hapo ijikusanye na ijikunjekunje na iseme, «Basi! Basi!» |