×

Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya majini! Hakika 6:128 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:128) ayat 128 in Swahili

6:128 Surah Al-An‘am ayat 128 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 128 - الأنعَام - Page - Juz 8

﴿وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا يَٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ قَدِ ٱسۡتَكۡثَرۡتُم مِّنَ ٱلۡإِنسِۖ وَقَالَ أَوۡلِيَآؤُهُم مِّنَ ٱلۡإِنسِ رَبَّنَا ٱسۡتَمۡتَعَ بَعۡضُنَا بِبَعۡضٖ وَبَلَغۡنَآ أَجَلَنَا ٱلَّذِيٓ أَجَّلۡتَ لَنَاۚ قَالَ ٱلنَّارُ مَثۡوَىٰكُمۡ خَٰلِدِينَ فِيهَآ إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٞ ﴾
[الأنعَام: 128]

Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu. Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana sisi na wao. Na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ويوم يحشرهم جميعا يامعشر الجن قد استكثرتم من الإنس وقال أولياؤهم من, باللغة السواحيلية

﴿ويوم يحشرهم جميعا يامعشر الجن قد استكثرتم من الإنس وقال أولياؤهم من﴾ [الأنعَام: 128]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na kumbuka, ewe Mtume, ile Siku Atakayowakusanya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, makafiri na wategemewa wao, miongoni mwa mashetani wa kijini, na kuwaambia, «Enyi mkusanyiko wa majini, hakika mumewapoteza binadamu wengi.» Na watasema wategemewa wao miongoni mwa makafiri wa kibinadamu, «EweMola wetu, kila mmoja katika sisi amenufaika na mwengine, na tumefikia kikomo ambacho umekiweka kwetu kwa kumalizika uhai wetu wa duniani.» Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Atasema Awaambie, «Moto ndio mashukio yenu, mtakaa milele, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu Ametaka asikaye milele,» miongoni mwa walioasi wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake na utengenezaji Wake, ni Mjuzi mno wa mambo yote ya waja Wake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek