Quran with Swahili translation - Surah Al-Mulk ayat 13 - المُلك - Page - Juz 29
﴿وَأَسِرُّواْ قَوۡلَكُمۡ أَوِ ٱجۡهَرُواْ بِهِۦٓۖ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ﴾
[المُلك: 13]
﴿وأسروا قولكم أو اجهروا به إنه عليم بذات الصدور﴾ [المُلك: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na yaficheni maneno yenu, enyi watu, katika jambo lolote miongoni mwa mambo yenu , au yadhihirisheni, kwani yote mawili mbele ya Mwenyezi Mungu ni sawa. Hakika Yeye , kutakasika ni Kwake, ni Mjuzi wa yaliyomo ndani ya vifua, basi yatafichamana vipi maneno yenu na matendo yenu Kwake Yeye |