Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 201 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ إِذَا مَسَّهُمۡ طَٰٓئِفٞ مِّنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ تَذَكَّرُواْ فَإِذَا هُم مُّبۡصِرُونَ ﴾
[الأعرَاف: 201]
﴿إن الذين اتقوا إذا مسهم طائف من الشيطان تذكروا فإذا هم مبصرون﴾ [الأعرَاف: 201]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika wale wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa viumbe wake, kwa kuogopa mateso Yake kwa kuzitekeleza faradhi Zake na kuyaepuka makatazo Yake, likiwapata tukio lolote la wasiwasi wa Shetani, wanayakumbuka yale Aliyowalazimisha Mwenyezi Mungu juu yao ya kumtii na kutubia Kwake, na punde si punde wanakomeka na kumuasi Mwenyezi Mungu wakiwa kwenye hoja ya wazi, wenye kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na wenye kumuasi Shetani |