×

Surah Al-Maarij in Swahili

Quran Swahili ⮕ Surah Maarij

Translation of the Meanings of Surah Maarij in Swahili - السواحيلية

The Quran in Swahili - Surah Maarij translated into Swahili, Surah Al-Maarij in Swahili. We provide accurate translation of Surah Maarij in Swahili - السواحيلية, Verses 44 - Surah Number 70 - Page 568.

بسم الله الرحمن الرحيم

سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ (1)
Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea
لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ (2)
Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia
مِّنَ اللَّهِ ذِي الْمَعَارِجِ (3)
Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja
تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ (4)
Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu
فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا (5)
Basi subiri kwa subira njema
إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا (6)
Hakika wao wanaiona iko mbali
وَنَرَاهُ قَرِيبًا (7)
Na Sisi tunaiona iko karibu
يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ (8)
Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa
وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ (9)
Na milima itakuwa kama sufi
وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا (10)
Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake
يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ (11)
Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe
وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ (12)
Na mkewe, na nduguye
وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ (13)
Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu
وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ (14)
Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye
كَلَّا ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ (15)
La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa
نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ (16)
Unao babua ngozi ya kichwa
تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ (17)
Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka
وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰ (18)
Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi
۞ إِنَّ الْإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا (19)
Hakika mtu ameumbwa na papara
إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا (20)
Inapo mgusa shari hupapatika
وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا (21)
Na inapo mgusa kheri huizuilia
إِلَّا الْمُصَلِّينَ (22)
Isipo kuwa wanao sali
الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ (23)
Ambao wanadumisha Sala zao
وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ (24)
Na ambao katika mali yao iko haki maalumu
لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ (25)
Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba
وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ (26)
Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo
وَالَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ (27)
Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi
إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ (28)
Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo
وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ (29)
Na ambao wanahifadhi tupu zao
إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ (30)
Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi
فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ (31)
Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka
وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ (32)
Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao
وَالَّذِينَ هُم بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ (33)
Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao
وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ (34)
Na ambao wanazihifadhi Sala zao
أُولَٰئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُّكْرَمُونَ (35)
Hao ndio watakao hishimiwa Peponi
فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ (36)
Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu
عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ (37)
Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto
أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ (38)
Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema
كَلَّا ۖ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ (39)
La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua
فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ (40)
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza
عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ (41)
Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi
فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ (42)
Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa
يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ (43)
Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo
خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ (44)
Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa
❮ Previous Next ❯

Surahs from Quran :

1- Fatiha2- Baqarah
3- Al Imran4- Nisa
5- Maidah6- Anam
7- Araf8- Anfal
9- Tawbah10- Yunus
11- Hud12- Yusuf
13- Raad14- Ibrahim
15- Hijr16- Nahl
17- Al Isra18- Kahf
19- Maryam20- TaHa
21- Anbiya22- Hajj
23- Muminun24- An Nur
25- Furqan26- Shuara
27- Naml28- Qasas
29- Ankabut30- Rum
31- Luqman32- Sajdah
33- Ahzab34- Saba
35- Fatir36- Yasin
37- Assaaffat38- Sad
39- Zumar40- Ghafir
41- Fussilat42- shura
43- Zukhruf44- Ad Dukhaan
45- Jathiyah46- Ahqaf
47- Muhammad48- Al Fath
49- Hujurat50- Qaf
51- zariyat52- Tur
53- Najm54- Al Qamar
55- Rahman56- Waqiah
57- Hadid58- Mujadilah
59- Al Hashr60- Mumtahina
61- Saff62- Jumuah
63- Munafiqun64- Taghabun
65- Talaq66- Tahrim
67- Mulk68- Qalam
69- Al-Haqqah70- Maarij
71- Nuh72- Jinn
73- Muzammil74- Muddathir
75- Qiyamah76- Insan
77- Mursalat78- An Naba
79- Naziat80- Abasa
81- Takwir82- Infitar
83- Mutaffifin84- Inshiqaq
85- Buruj86- Tariq
87- Al Ala88- Ghashiya
89- Fajr90- Al Balad
91- Shams92- Lail
93- Duha94- Sharh
95- Tin96- Al Alaq
97- Qadr98- Bayyinah
99- Zalzalah100- Adiyat
101- Qariah102- Takathur
103- Al Asr104- Humazah
105- Al Fil106- Quraysh
107- Maun108- Kawthar
109- Kafirun110- Nasr
111- Masad112- Ikhlas
113- Falaq114- An Nas