القرآن باللغة السواحيلية - سورة المعارج مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Maarij in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة المعارج باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 44 - رقم السورة 70 - الصفحة 568.

| سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ (1) Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea |
| لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ (2) Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia |
| مِّنَ اللَّهِ ذِي الْمَعَارِجِ (3) Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja |
| تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ (4) Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu |
| فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا (5) Basi subiri kwa subira njema |
| إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا (6) Hakika wao wanaiona iko mbali |
| وَنَرَاهُ قَرِيبًا (7) Na Sisi tunaiona iko karibu |
| يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ (8) Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa |
| وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ (9) Na milima itakuwa kama sufi |
| وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا (10) Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake |
| يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ (11) Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe |
| وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ (12) Na mkewe, na nduguye |
| وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ (13) Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu |
| وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ (14) Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye |
| كَلَّا ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ (15) La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa |
| نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ (16) Unao babua ngozi ya kichwa |
| تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ (17) Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka |
| وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰ (18) Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi |
| ۞ إِنَّ الْإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا (19) Hakika mtu ameumbwa na papara |
| إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا (20) Inapo mgusa shari hupapatika |
| وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا (21) Na inapo mgusa kheri huizuilia |
| إِلَّا الْمُصَلِّينَ (22) Isipo kuwa wanao sali |
| الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ (23) Ambao wanadumisha Sala zao |
| وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ (24) Na ambao katika mali yao iko haki maalumu |
| لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ (25) Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba |
| وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ (26) Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo |
| وَالَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ (27) Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi |
| إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ (28) Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo |
| وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ (29) Na ambao wanahifadhi tupu zao |
| إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ (30) Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi |
| فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ (31) Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka |
| وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ (32) Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao |
| وَالَّذِينَ هُم بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ (33) Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao |
| وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ (34) Na ambao wanazihifadhi Sala zao |
| أُولَٰئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُّكْرَمُونَ (35) Hao ndio watakao hishimiwa Peponi |
| فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ (36) Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu |
| عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ (37) Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto |
| أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ (38) Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema |
| كَلَّا ۖ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ (39) La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua |
| فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ (40) Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza |
| عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ (41) Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi |
| فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ (42) Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa |
| يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ (43) Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo |
| خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ (44) Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa |