Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 61 - الزُّمَر - Page - Juz 24
﴿وَيُنَجِّي ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ بِمَفَازَتِهِمۡ لَا يَمَسُّهُمُ ٱلسُّوٓءُ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ ﴾
[الزُّمَر: 61]
﴿وينجي الله الذين اتقوا بمفازتهم لا يمسهم السوء ولا هم يحزنون﴾ [الزُّمَر: 61]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mwenyezi Mungu Atawaokoa na Moto wa Jahanamu na adhabu yake wale waliomcha Mola wao kwa kutekeleza faradhi Alizoziamrisha na kujiepusha na yale Aliyoyakataza kwa kufuzu kwao na kutimia matakwa yao, nako ni kufaulu kupata Pepo. Hawataguswa na kitu chochote cha adhabu wala hawatazisikitikia hadhi za duniani walizozikosa |