Quran with Swahili translation - Surah An-Najm ayat 27 - النَّجم - Page - Juz 27
﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ تَسۡمِيَةَ ٱلۡأُنثَىٰ ﴾
[النَّجم: 27]
﴿إن الذين لا يؤمنون بالآخرة ليسمون الملائكة تسمية الأنثى﴾ [النَّجم: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika wale ambao hawaamini kuwa kuna maisha ya Akhera miongoni mwa makafiri wa Kiarabu wala hawafanyi matendo ya kuwafaa huko, wanawaita Malaika vile wanavyowaita wanawake, kwa kuitakidi kwao kuwa Malaika ni wanawake na kuwa wao ni watoto wa kike wa Mwenyezi Mungu |