Quran with Swahili translation - Surah Al-Qalam ayat 48 - القَلَم - Page - Juz 29
﴿فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلۡحُوتِ إِذۡ نَادَىٰ وَهُوَ مَكۡظُومٞ ﴾
[القَلَم: 48]
﴿فاصبر لحكم ربك ولا تكن كصاحب الحوت إذ نادى وهو مكظوم﴾ [القَلَم: 48]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi vumilia, ewe Mtume, kwa kile Alichokiamua Mola wako na kukipitisha. Na miongoni mwa hivyo ni kuwapa muhula na kuchelewesha ushindi wako kwao. Na usiwe ni kama yule mtu wa chewa, naye ni Yūnus, amani imshukie, alipokasirika na kutokuwa na uvumilivu na watu wake, pindi alipomuita Mola Wake, na huku amejawa na makero, akimuomba Awaharakishie adhabu |