×

Surah Al-Qalam in Swahili

Quran Swahili ⮕ Surah Qalam

Translation of the Meanings of Surah Qalam in Swahili - السواحيلية

The Quran in Swahili - Surah Qalam translated into Swahili, Surah Al-Qalam in Swahili. We provide accurate translation of Surah Qalam in Swahili - السواحيلية, Verses 52 - Surah Number 68 - Page 564.

بسم الله الرحمن الرحيم

ن ۚ وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ (1)
Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo
مَا أَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ (2)
Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu
وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ (3)
Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika
وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ (4)
Na hakika wewe una tabia tukufu
فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ (5)
Karibu utaona, na wao wataona
بِأَييِّكُمُ الْمَفْتُونُ (6)
Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ (7)
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka
فَلَا تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ (8)
Basi usiwat'ii wanao kadhibisha
وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ (9)
Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie
وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ (10)
Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa
هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ (11)
Mtapitapi, apitaye akifitini
مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ (12)
Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi
عُتُلٍّ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ (13)
Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu
أَن كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ (14)
Ati kwa kuwa ana mali na watoto
إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ (15)
Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani
سَنَسِمُهُ عَلَى الْخُرْطُومِ (16)
Tutamtia kovu juu ya pua yake
إِنَّا بَلَوْنَاهُمْ كَمَا بَلَوْنَا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ (17)
Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi
وَلَا يَسْتَثْنُونَ (18)
Wala hawakusema: Mungu akipenda
فَطَافَ عَلَيْهَا طَائِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَائِمُونَ (19)
Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala
فَأَصْبَحَتْ كَالصَّرِيمِ (20)
Likawa kama usiku wa giza
فَتَنَادَوْا مُصْبِحِينَ (21)
Asubuhi wakaitana
أَنِ اغْدُوا عَلَىٰ حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَارِمِينَ (22)
Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna
فَانطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ (23)
Basi walikwenda na huku wakinong'onezana
أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ (24)
Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni
وَغَدَوْا عَلَىٰ حَرْدٍ قَادِرِينَ (25)
Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo
فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ (26)
Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea
بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ (27)
Bali tumenyimwa
قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ (28)
Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu
قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ (29)
Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَاوَمُونَ (30)
Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao
قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ (31)
Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka
عَسَىٰ رَبُّنَا أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا رَاغِبُونَ (32)
Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi
كَذَٰلِكَ الْعَذَابُ ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ (33)
Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ (34)
Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi
أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ (35)
Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ (36)
Mna nini? Mnahukumu vipi
أَمْ لَكُمْ كِتَابٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ (37)
Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma
إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ (38)
Kuwa mtapata humo mnayo yapenda
أَمْ لَكُمْ أَيْمَانٌ عَلَيْنَا بَالِغَةٌ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۙ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ (39)
Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia
سَلْهُمْ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ (40)
Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya
أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ فَلْيَأْتُوا بِشُرَكَائِهِمْ إِن كَانُوا صَادِقِينَ (41)
Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli
يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ (42)
Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza
خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ وَقَدْ كَانُوا يُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ وَهُمْ سَالِمُونَ (43)
Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima
فَذَرْنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَٰذَا الْحَدِيثِ ۖ سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ (44)
Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua
وَأُمْلِي لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ (45)
Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara
أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ (46)
Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo
أَمْ عِندَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ (47)
Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika
فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ الْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ مَكْظُومٌ (48)
Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa
لَّوْلَا أَن تَدَارَكَهُ نِعْمَةٌ مِّن رَّبِّهِ لَنُبِذَ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ مَذْمُومٌ (49)
Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa
فَاجْتَبَاهُ رَبُّهُ فَجَعَلَهُ مِنَ الصَّالِحِينَ (50)
Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema
وَإِن يَكَادُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَارِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا الذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُ لَمَجْنُونٌ (51)
Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu
وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ (52)
Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote
❮ Previous Next ❯

Surahs from Quran :

1- Fatiha2- Baqarah
3- Al Imran4- Nisa
5- Maidah6- Anam
7- Araf8- Anfal
9- Tawbah10- Yunus
11- Hud12- Yusuf
13- Raad14- Ibrahim
15- Hijr16- Nahl
17- Al Isra18- Kahf
19- Maryam20- TaHa
21- Anbiya22- Hajj
23- Muminun24- An Nur
25- Furqan26- Shuara
27- Naml28- Qasas
29- Ankabut30- Rum
31- Luqman32- Sajdah
33- Ahzab34- Saba
35- Fatir36- Yasin
37- Assaaffat38- Sad
39- Zumar40- Ghafir
41- Fussilat42- shura
43- Zukhruf44- Ad Dukhaan
45- Jathiyah46- Ahqaf
47- Muhammad48- Al Fath
49- Hujurat50- Qaf
51- zariyat52- Tur
53- Najm54- Al Qamar
55- Rahman56- Waqiah
57- Hadid58- Mujadilah
59- Al Hashr60- Mumtahina
61- Saff62- Jumuah
63- Munafiqun64- Taghabun
65- Talaq66- Tahrim
67- Mulk68- Qalam
69- Al-Haqqah70- Maarij
71- Nuh72- Jinn
73- Muzammil74- Muddathir
75- Qiyamah76- Insan
77- Mursalat78- An Naba
79- Naziat80- Abasa
81- Takwir82- Infitar
83- Mutaffifin84- Inshiqaq
85- Buruj86- Tariq
87- Al Ala88- Ghashiya
89- Fajr90- Al Balad
91- Shams92- Lail
93- Duha94- Sharh
95- Tin96- Al Alaq
97- Qadr98- Bayyinah
99- Zalzalah100- Adiyat
101- Qariah102- Takathur
103- Al Asr104- Humazah
105- Al Fil106- Quraysh
107- Maun108- Kawthar
109- Kafirun110- Nasr
111- Masad112- Ikhlas
113- Falaq114- An Nas