The Quran in Swahili - Surah Waqiah translated into Swahili, Surah Al-Waqiah in Swahili. We provide accurate translation of Surah Waqiah in Swahili - السواحيلية, Verses 96 - Surah Number 56 - Page 534.

| إِذَا وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ (1) Litakapo tukia hilo Tukio |
| لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ (2) Hapana cha kukanusha kutukia kwake |
| خَافِضَةٌ رَّافِعَةٌ (3) Literemshalo linyanyualo |
| إِذَا رُجَّتِ الْأَرْضُ رَجًّا (4) Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso |
| وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسًّا (5) Na milima itapo sagwasagwa |
| فَكَانَتْ هَبَاءً مُّنبَثًّا (6) Iwe mavumbi yanayo peperushwa |
| وَكُنتُمْ أَزْوَاجًا ثَلَاثَةً (7) Na nyinyi mtakuwa namna tatu |
| فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ (8) Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani |
| وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ (9) Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni |
| وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ (10) Na wa mbele watakuwa mbele |
| أُولَٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ (11) Hao ndio watakao karibishwa |
| فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ (12) Katika Bustani zenye neema |
| ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ (13) Fungu kubwa katika wa mwanzo |
| وَقَلِيلٌ مِّنَ الْآخِرِينَ (14) Na wachache katika wa mwisho |
| عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ (15) Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa |
| مُّتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ (16) Wakiviegemea wakielekeana |
| يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ (17) Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele |
| بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ (18) Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi |
| لَّا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ (19) Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa |
| وَفَاكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ (20) Na matunda wayapendayo |
| وَلَحْمِ طَيْرٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ (21) Na nyama za ndege kama wanavyo tamani |
| وَحُورٌ عِينٌ (22) Na Mahurulaini |
| كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ (23) Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa |
| جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (24) Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda |
| لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا (25) Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi |
| إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا (26) Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama |
| وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ (27) Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani |
| فِي سِدْرٍ مَّخْضُودٍ (28) Katika mikunazi isiyo na miba |
| وَطَلْحٍ مَّنضُودٍ (29) Na migomba iliyo pangiliwa |
| وَظِلٍّ مَّمْدُودٍ (30) Na kivuli kilicho tanda |
| وَمَاءٍ مَّسْكُوبٍ (31) Na maji yanayo miminika |
| وَفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ (32) Na matunda mengi |
| لَّا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ (33) Hayatindikii wala hayakatazwi |
| وَفُرُشٍ مَّرْفُوعَةٍ (34) Na matandiko yaliyo nyanyuliwa |
| إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاءً (35) Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya |
| فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا (36) Na tutawafanya vijana |
| عُرُبًا أَتْرَابًا (37) Wanapendana na waume zao, hirimu moja |
| لِّأَصْحَابِ الْيَمِينِ (38) Kwa ajili ya watu wa kuliani |
| ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ (39) Fungu kubwa katika wa mwanzo |
| وَثُلَّةٌ مِّنَ الْآخِرِينَ (40) Na fungu kubwa katika wa mwisho |
| وَأَصْحَابُ الشِّمَالِ مَا أَصْحَابُ الشِّمَالِ (41) Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni |
| فِي سَمُومٍ وَحَمِيمٍ (42) Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka |
| وَظِلٍّ مِّن يَحْمُومٍ (43) Na kivuli cha moshi mweusi |
| لَّا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ (44) Si cha kuburudisha wala kustarehesha |
| إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُتْرَفِينَ (45) Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa |
| وَكَانُوا يُصِرُّونَ عَلَى الْحِنثِ الْعَظِيمِ (46) Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa |
| وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ (47) Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa |
| أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ (48) Au baba zetu wa zamani |
| قُلْ إِنَّ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ (49) Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho |
| لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ (50) Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu |
| ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ (51) Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha |
| لَآكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ (52) Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu |
| فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ (53) Na kwa mti huo mtajaza matumbo |
| فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ (54) Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka |
| فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ (55) Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu |
| هَٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ (56) Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo |
| نَحْنُ خَلَقْنَاكُمْ فَلَوْلَا تُصَدِّقُونَ (57) Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki |
| أَفَرَأَيْتُم مَّا تُمْنُونَ (58) Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza |
| أَأَنتُمْ تَخْلُقُونَهُ أَمْ نَحْنُ الْخَالِقُونَ (59) Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji |
| نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ الْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ (60) Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi |
| عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ أَمْثَالَكُمْ وَنُنشِئَكُمْ فِي مَا لَا تَعْلَمُونَ (61) Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua |
| وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ النَّشْأَةَ الْأُولَىٰ فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ (62) Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki |
| أَفَرَأَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ (63) Je! Mnaona makulima mnayo yapanda |
| أَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ (64) Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha |
| لَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَاهُ حُطَامًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ (65) Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu |
| إِنَّا لَمُغْرَمُونَ (66) Mkisema: Hakika sisi tumegharimika |
| بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ (67) Bali sisi tumenyimwa |
| أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاءَ الَّذِي تَشْرَبُونَ (68) Je! Mnayaona maji mnayo yanywa |
| أَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنزِلُونَ (69) Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha |
| لَوْ نَشَاءُ جَعَلْنَاهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ (70) Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru |
| أَفَرَأَيْتُمُ النَّارَ الَّتِي تُورُونَ (71) Je! Mnauona moto mnao uwasha |
| أَأَنتُمْ أَنشَأْتُمْ شَجَرَتَهَا أَمْ نَحْنُ الْمُنشِئُونَ (72) Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji |
| نَحْنُ جَعَلْنَاهَا تَذْكِرَةً وَمَتَاعًا لِّلْمُقْوِينَ (73) Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani |
| فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ (74) Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu |
| ۞ فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ (75) Basi naapa kwa maanguko ya nyota |
| وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ (76) Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua |
| إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ (77) Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu |
| فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ (78) Katika Kitabu kilicho hifadhiwa |
| لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ (79) Hapana akigusaye ila walio takaswa |
| تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ (80) Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote |
| أَفَبِهَٰذَا الْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ (81) Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza |
| وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ (82) Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha |
| فَلَوْلَا إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ (83) Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo |
| وَأَنتُمْ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ (84) Na nyinyi wakati huo mnatazama |
| وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ (85) Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi |
| فَلَوْلَا إِن كُنتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ (86) Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu |
| تَرْجِعُونَهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ (87) Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli |
| فَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُقَرَّبِينَ (88) Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa |
| فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ (89) Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema |
| وَأَمَّا إِن كَانَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ (90) Na akiwa katika watu wa upande wa kulia |
| فَسَلَامٌ لَّكَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ (91) Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia |
| وَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُكَذِّبِينَ الضَّالِّينَ (92) Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu |
| فَنُزُلٌ مِّنْ حَمِيمٍ (93) Basi karamu yake ni maji yanayo chemka |
| وَتَصْلِيَةُ جَحِيمٍ (94) Na kutiwa Motoni |
| إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ الْيَقِينِ (95) Hakika hii ndiyo haki yenye yakini |
| فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ (96) Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa |