×

Surah Adh-Dhariyat in Swahili

Quran Swahili ⮕ Surah zariyat

Translation of the Meanings of Surah zariyat in Swahili - السواحيلية

The Quran in Swahili - Surah zariyat translated into Swahili, Surah Adh-Dhariyat in Swahili. We provide accurate translation of Surah zariyat in Swahili - السواحيلية, Verses 60 - Surah Number 51 - Page 520.

بسم الله الرحمن الرحيم

وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوًا (1)
Naapa kwa pepo zinazo tawanya
فَالْحَامِلَاتِ وِقْرًا (2)
Na zinazo beba mizigo
فَالْجَارِيَاتِ يُسْرًا (3)
Na zinazo kwenda kwa wepesi
فَالْمُقَسِّمَاتِ أَمْرًا (4)
Na zinazo gawanya kwa amri
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ (5)
Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli
وَإِنَّ الدِّينَ لَوَاقِعٌ (6)
Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْحُبُكِ (7)
Naapa kwa mbingu zenye njia
إِنَّكُمْ لَفِي قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ (8)
Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana
يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ (9)
Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa
قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ (10)
Wazushi wameangamizwa
الَّذِينَ هُمْ فِي غَمْرَةٍ سَاهُونَ (11)
Ambao wameghafilika katika ujinga
يَسْأَلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ الدِّينِ (12)
Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo
يَوْمَ هُمْ عَلَى النَّارِ يُفْتَنُونَ (13)
Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni
ذُوقُوا فِتْنَتَكُمْ هَٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ (14)
Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ (15)
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem
آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ (16)
Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema
كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ (17)
Walikuwa wakilala kidogo tu usiku
وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ (18)
Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira
وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ (19)
Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba
وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ (20)
Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini
وَفِي أَنفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ (21)
Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni
وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ (22)
Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa
فَوَرَبِّ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ (23)
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ (24)
Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa
إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ (25)
Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni
فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ (26)
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona
فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ (27)
Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli
فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ (28)
Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu
فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُهُ فِي صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ (29)
Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa
قَالُوا كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ (30)
Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua
۞ قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ (31)
AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa
قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ (32)
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu
لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن طِينٍ (33)
Tuwatupie mawe ya udongo
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ (34)
Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka
فَأَخْرَجْنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ (35)
Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini
فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِّنَ الْمُسْلِمِينَ (36)
Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu
وَتَرَكْنَا فِيهَا آيَةً لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ الْعَذَابَ الْأَلِيمَ (37)
Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu
وَفِي مُوسَىٰ إِذْ أَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ (38)
Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi
فَتَوَلَّىٰ بِرُكْنِهِ وَقَالَ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ (39)
Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu
فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ (40)
Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa
وَفِي عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الرِّيحَ الْعَقِيمَ (41)
Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi
مَا تَذَرُ مِن شَيْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَالرَّمِيمِ (42)
Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka
وَفِي ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا حَتَّىٰ حِينٍ (43)
Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu
فَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ (44)
Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona
فَمَا اسْتَطَاعُوا مِن قِيَامٍ وَمَا كَانُوا مُنتَصِرِينَ (45)
Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ (46)
Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu
وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ (47)
Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua
وَالْأَرْضَ فَرَشْنَاهَا فَنِعْمَ الْمَاهِدُونَ (48)
Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi
وَمِن كُلِّ شَيْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ (49)
Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie
فَفِرُّوا إِلَى اللَّهِ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ (50)
Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake
وَلَا تَجْعَلُوا مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ (51)
Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake
كَذَٰلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ (52)
Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu
أَتَوَاصَوْا بِهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ (53)
Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَا أَنتَ بِمَلُومٍ (54)
Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi
وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ (55)
Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ (56)
Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi
مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ (57)
Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe
إِنَّ اللَّهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ (58)
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti
فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذَنُوبًا مِّثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَابِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ (59)
Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن يَوْمِهِمُ الَّذِي يُوعَدُونَ (60)
Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa
❮ Previous Next ❯

Surahs from Quran :

1- Fatiha2- Baqarah
3- Al Imran4- Nisa
5- Maidah6- Anam
7- Araf8- Anfal
9- Tawbah10- Yunus
11- Hud12- Yusuf
13- Raad14- Ibrahim
15- Hijr16- Nahl
17- Al Isra18- Kahf
19- Maryam20- TaHa
21- Anbiya22- Hajj
23- Muminun24- An Nur
25- Furqan26- Shuara
27- Naml28- Qasas
29- Ankabut30- Rum
31- Luqman32- Sajdah
33- Ahzab34- Saba
35- Fatir36- Yasin
37- Assaaffat38- Sad
39- Zumar40- Ghafir
41- Fussilat42- shura
43- Zukhruf44- Ad Dukhaan
45- Jathiyah46- Ahqaf
47- Muhammad48- Al Fath
49- Hujurat50- Qaf
51- zariyat52- Tur
53- Najm54- Al Qamar
55- Rahman56- Waqiah
57- Hadid58- Mujadilah
59- Al Hashr60- Mumtahina
61- Saff62- Jumuah
63- Munafiqun64- Taghabun
65- Talaq66- Tahrim
67- Mulk68- Qalam
69- Al-Haqqah70- Maarij
71- Nuh72- Jinn
73- Muzammil74- Muddathir
75- Qiyamah76- Insan
77- Mursalat78- An Naba
79- Naziat80- Abasa
81- Takwir82- Infitar
83- Mutaffifin84- Inshiqaq
85- Buruj86- Tariq
87- Al Ala88- Ghashiya
89- Fajr90- Al Balad
91- Shams92- Lail
93- Duha94- Sharh
95- Tin96- Al Alaq
97- Qadr98- Bayyinah
99- Zalzalah100- Adiyat
101- Qariah102- Takathur
103- Al Asr104- Humazah
105- Al Fil106- Quraysh
107- Maun108- Kawthar
109- Kafirun110- Nasr
111- Masad112- Ikhlas
113- Falaq114- An Nas