| الرَّحْمَٰنُ (1) Arrah'man, Mwingi wa Rehema
 | 
| عَلَّمَ الْقُرْآنَ (2) Amefundisha Qur'ani
 | 
| خَلَقَ الْإِنسَانَ (3) Amemuumba mwanaadamu
 | 
| عَلَّمَهُ الْبَيَانَ (4) Akamfundisha kubaini
 | 
| الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ (5) Jua na mwezi huenda kwa hisabu
 | 
| وَالنَّجْمُ وَالشَّجَرُ يَسْجُدَانِ (6) Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea
 | 
| وَالسَّمَاءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ الْمِيزَانَ (7) Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani
 | 
| أَلَّا تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ (8) Ili msidhulumu katika mizani
 | 
| وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ (9) Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani
 | 
| وَالْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ (10) Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe
 | 
| فِيهَا فَاكِهَةٌ وَالنَّخْلُ ذَاتُ الْأَكْمَامِ (11) Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba
 | 
| وَالْحَبُّ ذُو الْعَصْفِ وَالرَّيْحَانُ (12) Na nafaka zenye makapi, na rehani
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (13) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| خَلَقَ الْإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ كَالْفَخَّارِ (14) Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo
 | 
| وَخَلَقَ الْجَانَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ (15) Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (16) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ (17) Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (18) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ (19) Anaziendesha bahari mbili zikutane
 | 
| بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَّا يَبْغِيَانِ (20) Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (21) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ (22) Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (23) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| وَلَهُ الْجَوَارِ الْمُنشَآتُ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ (24) Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (25) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ (26) Kila kilioko juu yake kitatoweka
 | 
| وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ (27) Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (28) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| يَسْأَلُهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ (29) Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (30) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ الثَّقَلَانِ (31) Tutakuhisabuni enyi makundi mawili
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (32) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَن تَنفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانفُذُوا ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ (33) Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (34) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِّن نَّارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنتَصِرَانِ (35) Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (36) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| فَإِذَا انشَقَّتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَالدِّهَانِ (37) Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (38) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُسْأَلُ عَن ذَنبِهِ إِنسٌ وَلَا جَانٌّ (39) Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (40) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ (41) Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (42) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| هَٰذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا الْمُجْرِمُونَ (43) Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha
 | 
| يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ آنٍ (44) Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (45) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ (46) Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (47) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| ذَوَاتَا أَفْنَانٍ (48) Bustani zenye matawi yaliyo tanda
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (49) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ (50) Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (51) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| فِيهِمَا مِن كُلِّ فَاكِهَةٍ زَوْجَانِ (52) Humo katika kila matunda zimo namna mbili
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (53) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ فُرُشٍ بَطَائِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ ۚ وَجَنَى الْجَنَّتَيْنِ دَانٍ (54) Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (55) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ (56) Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (57) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| كَأَنَّهُنَّ الْيَاقُوتُ وَالْمَرْجَانُ (58) Kama kwamba wao ni yakuti na marijani
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (59) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ (60) Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (61) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ (62) Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (63) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| مُدْهَامَّتَانِ (64) Za kijani kibivu
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (65) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ (66) Na chemchem mbili zinazo furika
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (67) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| فِيهِمَا فَاكِهَةٌ وَنَخْلٌ وَرُمَّانٌ (68) Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (69) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| فِيهِنَّ خَيْرَاتٌ حِسَانٌ (70) Humo wamo wanawake wema wazuri
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (71) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| حُورٌ مَّقْصُورَاتٌ فِي الْخِيَامِ (72) Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (73) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ (74) Hajawagusa mtu wala jini kabla yao
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (75) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ رَفْرَفٍ خُضْرٍ وَعَبْقَرِيٍّ حِسَانٍ (76) Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri
 | 
| فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (77) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
 | 
| تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ (78) Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu
 |