| إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ (1) Jua litakapo kunjwa
 | 
| وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ (2) Na nyota zikazimwa
 | 
| وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ (3) Na milima ikaondolewa
 | 
| وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ (4) Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe
 | 
| وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ (5) Na wanyama wa mwituni wakakusanywa
 | 
| وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ (6) Na bahari zikawaka moto
 | 
| وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ (7) Na nafsi zikaunganishwa
 | 
| وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ (8) Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa
 | 
| بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ (9) Kwa kosa gani aliuliwa
 | 
| وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ (10) Na madaftari yatakapo enezwa
 | 
| وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ (11) Na mbingu itapo tanduliwa
 | 
| وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ (12) Na Jahannamu itapo chochewa
 | 
| وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ (13) Na Pepo ikasogezwa
 | 
| عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ (14) Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha
 | 
| فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ (15) Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma
 | 
| الْجَوَارِ الْكُنَّسِ (16) Zinazo kwenda, kisha zikajificha
 | 
| وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ (17) Na kwa usiku unapo pungua
 | 
| وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ (18) Na kwa asubuhi inapo pambazuka
 | 
| إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ (19) Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu
 | 
| ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ (20) Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi
 | 
| مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ (21) Anaye t'iiwa, tena muaminifu
 | 
| وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ (22) Na wala huyu mwenzenu hana wazimu
 | 
| وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ (23) Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi
 | 
| وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ (24) Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu
 | 
| وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ (25) Wala hii si kauli ya Shetani maluuni
 | 
| فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ (26) Basi mnakwenda wapi
 | 
| إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ (27) Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote
 | 
| لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ (28) Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa
 | 
| وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ (29) Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote
 |