وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا (1) Naapa kwa jua na mwangaza wake |
وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا (2) Na kwa mwezi unapo lifuatia |
وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا (3) Na kwa mchana unapo lidhihirisha |
وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا (4) Na kwa usiku unapo lifunika |
وَالسَّمَاءِ وَمَا بَنَاهَا (5) Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga |
وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا (6) Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza |
وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا (7) Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza |
فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا (8) Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake |
قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا (9) Hakika amefanikiwa aliye itakasa |
وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا (10) Na hakika amekhasiri aliye iviza |
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا (11) Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao |
إِذِ انبَعَثَ أَشْقَاهَا (12) Alipo simama mwovu wao mkubwa |
فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ نَاقَةَ اللَّهِ وَسُقْيَاهَا (13) Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake |
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنبِهِمْ فَسَوَّاهَا (14) Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa |
وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا (15) Wala Yeye haogopi matokeo yake |