لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ (1) Ninaapa kwa Siku ya Kiyama |
وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ (2) Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu |
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ (3) Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake |
بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ (4) Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake |
بَلْ يُرِيدُ الْإِنسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ (5) Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake |
يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ (6) Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama |
فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ (7) Basi jicho litapo dawaa |
وَخَسَفَ الْقَمَرُ (8) Na mwezi utapo patwa |
وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ (9) Na likakusanywa jua na mwezi |
يَقُولُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ (10) Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio |
كَلَّا لَا وَزَرَ (11) La! Hapana pa kukimbilia |
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمُسْتَقَرُّ (12) Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu |
يُنَبَّأُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ (13) Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha |
بَلِ الْإِنسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ (14) Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake |
وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ (15) Na ingawa atatoa chungu ya udhuru |
لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ (16) Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka |
إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ (17) Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha |
فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ (18) Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake |
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ (19) Kisha ni juu yetu kuubainisha |
كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ (20) Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani |
وَتَذَرُونَ الْآخِرَةَ (21) Na mnaacha maisha ya Akhera |
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ (22) Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara |
إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ (23) Zinamwangallia Mola wao Mlezi |
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ بَاسِرَةٌ (24) Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana |
تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ (25) Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo |
كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ (26) La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo |
وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ (27) Na pakasemwa: Nani wa kumganga |
وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ (28) Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki |
وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ (29) Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi |
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمَسَاقُ (30) Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi |
فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ (31) Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali |
وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ (32) Bali alikanusha, na akageuka |
ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰ أَهْلِهِ يَتَمَطَّىٰ (33) Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao |
أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ (34) Ole wako, ole wako |
ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ (35) Kisha Ole wako, ole wako |
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى (36) Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure |
أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ (37) Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa |
ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ (38) Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo |
فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ (39) Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke |
أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ (40) Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu |