القرآن باللغة السواحيلية - سورة المرسلات مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Mursalat in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة المرسلات باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 50 - رقم السورة 77 - الصفحة 580.
وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا (1) Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole |
فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا (2) Na zinazo vuma kwa kasi |
وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا (3) Na zikaeneza maeneo yote |
فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا (4) Na zinazo farikisha zikatawanya |
فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا (5) Na zinazo peleka mawaidha |
عُذْرًا أَوْ نُذْرًا (6) Kwa kuudhuru au kuonya |
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ (7) Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa |
فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ (8) Wakati nyota zitakapo futwa |
وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ (9) Na mbingu zitakapo pasuliwa |
وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ (10) Na milima itakapo peperushwa |
وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ (11) Na Mitume watakapo wekewa wakati wao |
لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ (12) Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo |
لِيَوْمِ الْفَصْلِ (13) Kwa siku ya kupambanua |
وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ (14) Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (15) Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha |
أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ (16) Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia |
ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ (17) Kisha tukawafuatilizia walio fuatia |
كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ (18) Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (19) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha |
أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ (20) Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa |
فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ (21) Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti |
إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ (22) Mpaka muda maalumu |
فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ (23) Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (24) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha |
أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا (25) Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya |
أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا (26) Walio hai na maiti |
وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاءً فُرَاتًا (27) Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (28) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha |
انطَلِقُوا إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ (29) Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha |
انطَلِقُوا إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ (30) Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu |
لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّهَبِ (31) Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako |
إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ (32) Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba |
كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ (33) Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (34) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha |
هَٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ (35) Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu |
وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ (36) Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (37) Ole wao siku hiyo hao walio kanusha |
هَٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ (38) Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia |
فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ (39) Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (40) Ole wao siku hiyo hao walio kanusha |
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ (41) Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem |
وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ (42) Na matunda wanayo yapenda |
كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ (43) Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda |
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (44) Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (45) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha |
كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ (46) Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (47) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha |
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ (48) Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (49) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha |
فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ (50) Basi maneno gani baada ya haya watayaamini |